Baraka FM

Dkt.Tulia apokelewa kwa shangwe Mbeya

13 November 2023, 18:50

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Comrade Juma Homera akisalimiana na Dkt. Tulia Ackson katika mapokezi ya kumpongeza kushinda kiti cha urais wa umoja wa mabunge duniani IPU (picha na Hobokela Lwinga)

Na Hobokela Lwinga

Mapokezi ya spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na rais wa umoja wa mabunge duniani Dkt. Tulia Ackson mkoani Mbeya hasa jimboni kwake Mbeya mjini yamefanyika kwa kishindo na ubora mkubwa. Wakati hafla hiyo ya mapokezi ikiendelea mkuu wa mkoa wa Mbeya Comrade Juma Homera akapata nafasi ya kuzungumza.

Katika hotuba yake RC Homera mbali na kutaja miradi iliyotekelezwa na serikali ya awamu ya sita ya Chama Cha Mapinduzi chini ya mama Samia Suluhu Hassan lakini pia amewaasa wananchi mkoani Mbeya kumwona Dkt.Tulia kama tunu waliyopewa na Mungu na kuacha tabia ya kumnenea mabaya.

Homera amesema nafasi aliyoipata Dkt.Tulia ni fahari kwa wana-mbeya na Nyanya za Juu Kusini hivyo ni vema wakajikita katika kumwombea ili aendelee kuwatumikia na kuwaletea maendeleo ndani ya jimbo la Mbeya.

Aidha RC Homera ameendelea kuwaonya wale wote wanaotaka kuigeuza Mbeya kama kitovu cha vurugu na fujo zinazofifiza amani kwa wananchi kuacha mara moja kwa kuwa hatoweza kuvumilia yeyote atakayebainika.

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Comrade Juma Homera
Sauti ya Mkuu wa mkoa wa Mbeya Comrade Juma Homera