Baraka FM

TCRA kuwachukulia hatua wapandisha bei ya vocha kiholela

6 June 2024, 15:27

Meneja wa TCRA kanda ya nyanda za juu bw.Bonface Shoo(picha na Hobokela Lwinga)

Wakati mtaani malalamiko yakiendelea kuwa mengi kuhusiana na kupanda kwa vocha wananchi wanapaswa kutoa taarifa kwa wahusika na wasimamizi wa mawasiliano nchini.

Na Hobokela Lwinga

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini imewataka wauzaji wa vocha kuacha kupandisha bei za vocha kiholela na watakaobainika watachukuliwa hatua za kisheria.

Wito huo umetolewa na Meneja wa TCRA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Bw. Bonface Shoo wakati akizungumza na kituo hiki katika kipindi cha jarida kinachorushwa na kituo cha redio Baraka FM.

Meneja wa TCRA kanda ya nyanda za juu bw.Bonface Shoo (Picha na Hobokela Lwinga)
Meneja wa TCRA kanda ya nyanda za juu bw.Bonface Shoo

Shoo amesema waliopandisha vocha sio makampuni bali ni mawakala ambao wameamua kuvunja kanuni na sheria .

Aidha meneja huyo amewataka wananchi wanaokumbana na kero hiyo kutoa taarifa ili kuweza kuwabaini wauzaji wanaouza kinyume na utaratibu sambamba na kuwataka watumiaji wavocha kutumia huduma za kifedha kununua vifurushi ili kuondokana na kero hiyo.

Meneja wa TCRA kanda ya nyanda za juu bw.Bonface Shoo