Baraka FM

Naibu waziri Mwinjuma afunga kongamano la idhaa za kiswahili duniani Mbeya

22 March 2024, 17:49

Naibu Waziri wa utamaduni sanaa na michezo akifunga kongamano la nne la idha za kiswahili duniani(picha na Hobokela Lwinga)

Wahenga wanasema elimu haina mwisho,inapotokea fursa hupaswi kuiacha kwani hiyo inakuwa na moja ya kujiongezea maarifa.

Na Hobokela Lwinga

Naibu waziri wa utamaduni Sanaa na michezo Mhe. HAMIS MWINJUMA amesema lugha ya Kiswahili ni kiungo muhimu cha mawasiliano miongoni mwa watu wanaofanya shughuli za uchumi wa buluu  katika nchi yetu na Nchi nyingine.

wakufunzi wa kongamano la idha za kiswahili wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Mhe. Hamis Mwinjuma akifunga kongamano hilo(picha na Hobokela Lwinga)
Sauti ya Naibu waziri Hamis Mwinjuma

Mhe.Mwinjuma ameyasema hayo leo wakati akifunga kongamano la nne la idhaa za Kiswahili duniani lililofanyika jijini Mbeya.

Aidha Mhe.Mwinjuma amevitaka vyombo vya habari kutumia   misamiati inayofaa katika kutoa habari ili wasikilizaji wajifunze Kiswahili fasaha ili kiendelee kuenea Zaidi ulimwenguni.

Sauti ya Naibu waziri utamadi sanaa na michezo

Nae amesema taifa linatekeleza mkakati wa taifa wa kubidhaisha Kiswahili ambao ulianza mwaka 2022  na utaitimishwa rasmi mwaka 2032.

Katibu Mtendaji  wa Baraza la Kiswahili Taifa (BAKITA) Bi.Consolata Mushi(Hobokela Lwinga)
sauti ya Katibu Mtendaji  wa Baraza la Kiswahili Taifa (BAKITA) Bi.Consolata Mushi

Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mbarack Batenga amewata watanzania   kuendelea kuenzi, kukikuza na kukibidhaisha kiswahili  kama nyenzo ya kukuza na kuendeleza ustawi wMkuu wa Wilaya ya Chunya Mbarack Batengaa jamii na uchumi.

Suti ya Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mbarack Batenga

Nao baadhi ya washiriki wa kongamano hilo wameeleza namna walivyo nufaika na mafunzo hayo.

baadhi ya washiriki wa kongamano la nne la idha za kiswahili duniani(Hobokela Lwinga)
Sauti za baadhi ya washiriki wa kongamano

Kongamano la nne la idhaa za Kiswahili duniani lilianza tarehe 18 march 2024 na kufungwa ijumaahii ya march 22 likiwa na kauli mbiu:Tasnia ya habari na fursa za ubidhaishaji kiswahili duniani.