Baraka FM

Diwani Mariam:Wawepo wataalamu wa saikolojia kwenye kata

7 March 2024, 15:57

picha ya pamoja washiriki wa semina na viongozi (picha na Hobokela Lwinga)

Mamilioni ya watanzania wanajihususha na ujasiriamali mdogo hali inayo wafanya wajiingizie kipato kutokana na hilo hawana budii kupata elimu inayowawezesha kufanya shughuli zao kwa weledi.

Na Hobokela Lwinga

Kuelekea kilele cha siku ya mwanamke duniani,diwani wa viti maalum jiji la Mbeya Mariam Jason ameshauri kuwepo na wataalamu wa saikolojia kuanzia ngazi ya kata ili kuondoa au kupunguza matatizo ya magonjwa ya akili yanayoikabili jamii.

Ushauri huo ameutoa akiwa mgeni rasmi katika semina ya ujasiriamali iliyoandaliwa na kampuni ya mama kansolele products iliyofanyika katika ukumbi wa chuo  cha maendeleo ya jamii uyole jijini Mbeya.

diwani wa viti maalum jiji la Mbeya Mariam Jason(picha na Hobokela Lwinga)
Sauti ya diwani wa viti maalum jiji la mbeya Mariam Jason

Wakati akifundisha kwenye semina hiyo msaikolojia kutoka hospitali ya rufaa kanda ya Mbeya Yisambi Mbuwi Ndagamsu amesema unapofanya biashara yoyote unapaswa kuwa na nidhamu ya fedha.

Msaikolojia kutoka hospitali ya rufaa kanda ya Mbeya Yisambi Mbuwi Ndagamsu(picha na Hobokela Lwinga)
Sauti ya msaikolojia kutoka hospitali ya rufaa kanda ya Mbeya Yisambi Mbuwi Ndagamsu

Awali akisoma risala kwa mgeni rasmi mkurugenzi wa Mama Kansolele Products Hamisa Abdalah Juma amesema lengo la semina ambazo wanaziandaa zinalengo la kumsaidia kila mtu kukua kiuchumi.

Mkurugenzi wa Mama Kansolele Products Hamisa Abdalah Juma(picha na Hobokela Lwinga)
Sauti ya mkurugenzi wa Mama Kansolele Products Hamisa Abdalah Juma

Baadhi ya washiriki katika semina hiyo wamesema wajasiriamali wanatakiwa kuwa wabunifu kwenye shughuli zao wanazofanya za kuwaingizia kipato huku wakiwashukru waandaaji wa semina hiyo.

Baadhi ya washiriki wa semina (picha na Hobokela Lwinga)
Sauti za Baadhi ya washiriki wa semina

Kauli Ya Siku Ya Mwanamke Duniani Inasema “Wekeza Kwa Mwanamke Kuharakisha Maendeleo Ya Taifa“