Baraka FM

Tupo tayari kuboresha utalii nchini -REGROW

14 September 2023, 20:00

baadhi ya wananchi wa kabila la wamasai wakifurahia kitoweo(picha na Moses Mbwambo)

Wahenga wanasema jasiri haachi asili hivyo ndivyo unaweza kusema kutokana na kile ambacho kimekuwa kikifanywa na wizara ya maliasili na utalii nchini Tanzania kutokana na kudumisha mila na destri  ya mtanzania hasa katika kuenzi ngoma za asili na vyakula kwa kila kabila.

Na Moses Mbwambo

Wizara ya Maliasili na Utalii nchini kupitia mradi wa Kuboresha usimamizi wa Maliasili na kukuza Utalii Nyanda za juu Kusini (REGROW) imechagiza uanzishwaji wa vikundi vya kijamii vilivyoanzisha mazao mapya ya Utalii kama vile ngoma za asili,vyakula vya asili, bidhaa za kiutamaduni kwa lengo la kuinua wananchi kiuchumi pamoja na ulinzi wa Maliasili nchini.

Akizungumza kwa niaba ya wanakikundi wa jamii ya Kabila la Kimasai, vinavyowezeshwa na Mradi wa REGROW, Bw. Madicini Matayani, amesema Watalii wanapoenda au kutoka katika Hifadhi ya Taifa Ruaha wanapitia kwenye vikundi vyao na kufurahia Utalii wa kiutamaduni hususani ngoma, nyama inayochomwa kiasili, Mavazi ya asili nk.

Bw. Matayani ameongeza kuwa kutokana na fedha wanazozipata kutoka kwa Watalii maisha ya familia zao yamebadilika na sasa wanamiliki nyumba za kisasa, wanasomesha watoto, wananunua chakula cha uhakika na kuchangia katika uchumi wa nchi.

Baadhi ya wanufaika wa NEGROW wakifurahia mafaniko waliyoyapata kutoka NEGROW(Picha na Moses Mbwambo)

Wanufaika wengine wa Mradi kutoka Kikundi cha Tembo Pilipili kijijini hapo wameeleza kufurahishwa na mradi huo kwani kwasasa wameweza kusaidia kuimarisha shughuli za uhifadhi pamoja na kuwa marafiki wa Wanyamapori kwa kuandaa njia rafiki za kudhibiti Tembo kuingia katika makazi ya watu na kuharibu mazao yao kupitia mbinu za asili.

Wanakikundi cha uzalishaji wa zao la pilipili na wanufaika wa NEGROW wakionyesha namna ambavyo zao hilo limekuwa msaada kwao kiuchumi(Picha na Moses Mbwambo)

Akizungumzia Mradi huo, Naibu Msimamizi wa Mradi wa REGROW, Bi. Blanka Tengia amebainisha kuwa, mradi huo unatekelezwa kwenye Hifadhi nne, ambazo ni Hifadhi ya Taifa Ruaha, Hifadhi ya Taifa Nyerere, Hifadhi ya Taifa Mikumi na Hifadhi ya Taifa Milima ya Udzungwa na kuwa  REGROW umekusudia kuimarisha uhifadhi wa Ikolojia na kuwezesha jamii kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Baadhi ya waakilishi kutoka wizara ya mali asili na utalii wakiwa pamoja na baadhi ya wanavikundi waliochini ya NEGROW(picha na Moses Mbwambo)