Baraka FM

Matinyi: Shirikianeni na vyombo vya habari kueleza kazi zinazofanywa na serikali

31 January 2024, 19:14

Msemaji mkuu wa serikali Mobhare Matinyi(picha na Hobokela Lwinga)

Na Hobokela Lwinga

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera amesema jengo jipya liliojengwa na serikali katika hospitali ya wazazi Kanda ya Mbeya “Meta“  linahudumia zaidi ya wanawake wajawazito 200.

Hayo yamebainishwa katika mkutano na waandishi wa habari uliondaliwa idara ya habari maelezo kwa kushirikiana na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mbeya yenye lengo la uwasilishwaji wa taarifa za miradi ya maendeleo inayofanyika katika mkoa wa mbeya.

Homera amesema mkoa umetekeleza miradi mbalimbali ikiwemo katika sekta ya afya,elimu,maji,kilimo,miundombinu ya barabara pamoja na usafiri wa anga.

Sauti ya Mkuu wa mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera

Nao baadhi ya wakurugenzi katika halmashauri za mkoa wa mbeya wamemeishukru serikali kuendelea kutoa fedha za maendeleo huku wakiahidi kuendelea kusimamia kwa weledi.

Baadhi ya wakurugenzi katika halmashauri za mkoa wa Mbeya

Hata hivyo msemaji mkuu wa serikali Mobhare Matinyi amewashauri wakurugenzi kuwa na ushirikiano mzuri na vyombo vya habari na kuvitumia kuelezea miradi inayotekelezwa na serikali kwenye maeneo yao.

Sauti ya msemaji mkuu wa serikali Mobhare Matinyi