Baraka FM

Madiwani wanawake watembelea miradi ya maji Mbeya

20 March 2024, 18:55

Sehemu ya ujenzi wa mradi wa maji unaojengwa katika kijiji cha Ilunga halmashauri ya Mbeya.(picha na Sifael Kyonjola)

Kutokana na changamoto ya uhaba wa maji kwa baadhi ya wakazi jijini Mbeya mamlaka ya maji safi imeendelea kujenga miradi ya maji ili kunusuru hali hiyo.

Na Sifael Kyonjola

Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Mbeya kwa kushirikiana na madiwani wa kuteuliwa imefanya ziara katika vyanzo viwili vipya vya maji ambavyo vinatarajiwa kuanza kutumika mwishoni mwa mwezi huu.

Neema Stanton amesema lengo kuu la ziara hiyo ni kutoa elimu kwa viongozi hao namna bora ya kutumia maji ili kuepuka malalamiko ya wateja kubambikiziwa ankara kubwa za maji.

sauti ya afisa uhusiano idara ya maji Neema Stanton

Mmoja wa madiwani hao Atupele Msai amesema madiwani hao wanawake wanaishukuru serikali ya Dkt.Samia Suluhu Hassan kutoa fedha na kutekeleza miradi ya maji ya Itagano na Ulunga itakayomaliza tatizo la maji katika kata mbalimbali za mji wa Mbeya na Mbeya vijijini.

katikati ni Diwani Atupele Msai akitoa shukrani kwa serikali(picha na Sifael Kyonjola)
Sauti ya Atupele Msai diwani akitoa shukrani kwaniaba ya madiwani

Nae Mhandisi wa mamlaka hiyo Deogratius Leonidaamesema miradi hiyo imekamilika kwa asilimia tisini na tano.

mdiwani wakiendelea na ukaguzi wa miradi (picha Sifael Kyonjola)