Baraka FM

Diwani Iyunga agawa jezi sekondari ya Lupeta Mbeya

8 November 2023, 14:31

Wananfunzi wa shule za  sekondari mkoani  mbeya wametakiwa  kusoma kwa bidii na kushika yale yote yanayo fundishwa  na walimu wao ili yaweze  kuwasaidia.

Na Iman Anyigulile

Hayo yameelezwa na mh diwani wa kata ya Iyunga Mwajuma Tindwa wakati alipokuwa akikabidhi jezi kwa wanafunzi wa shule ya sekondari lupeta iliyopo kata ya iyunga jijini mbeya

Mh Tindwa amesema kuwa  msaada huo alio utoa amewaahidi wananfunzi hao na hivyo kuweza kutekeleza ahadi hiyo ili wanafunzi waendelee kufanya vizuri katika  idara ya michezo.

Mh diwani wa kata ya Iyunga Mwajuma Tindwa (kulia)akiwa katika shule ya Sekondari ya Lupeta(picha na Iman Anyigulile)
Mh diwani wa kata ya Iyunga Mwajuma Tindwa

Kwa upande wake afisa mtendaji wa kata ya Iyunga  Jacksoni  Yusuph ametumia nafasi hiyo kumshukuru diwani kwa kuwa  amekua akitimiza ahadi zake kwa vitendo.

Sauti ya Afisa mtendaji wa kata ya Iyunga  Jackson  Yusuph

Mkuu wa shule ya sekondari lupeta Nikumwitika  Kashililika  amemshukuru  mh diwani kwa msaada huo huku akiahidi kuwa watafanya vizuri katika  sekta ya michezo.

Sauti ya Mkuu wa shule ya sekondari lupeta Nikumwitika  Kashililika 

Nae mwalimu wa michezo wa shule hiyo Stella  Mkondya   amemwahidi mh diwani kuwa  wana amini wakati ujao watakua na matokeo mazuri katika  michezo ya umiseta.

Sauti ya mwalimu wa michezo wa shule hiyo Stella  Mkondya 

.