Baraka FM

Mwanamke afariki akielekea kutibiwa hospitali

28 November 2023, 11:48

Na Frola Godwin

Mwananke mmoja anayejulikana kwa majina ya Selina Kasekwa (69)amekutwa amefari katika mashamba ya Tazara yaliyopo Ikuti Iyunga jijini Mbeya.

Wakizungumza na kituo hiki baadhi ya mashuhuda wamedai marehemu alikuwa mgonjwa hivyo kifo chake kimetokea wakati akijipeleka hospitali bila msaada wa ndugu.

Aidha wananchi hao wamelitupia lawama jeshi la polisi kwa kuwa na mwamko mdogo wa kufika kwenyetukio hili licha ya kupewa taarifa kwa wakati.

Sauti za baadhi ya mashuhuda

Hata hivyo mwenyekiti wa mtaa huo Nelson Mahena amesema marehemu huyo ametambilika na ndugu zake na mwili wake umechukuliwa kwa ajili ya taratibu za maziko.

Pia Mahena amewataka wananchi kutokuwaacha wagonjwa pekee yao badala yake amewataka wawe karibu na kuweza kuwasaidia.

Sauti ya mwenyekiti wa mtaa huo Nelson Mahena