Baraka FM

Ugomvi wa wazazi mbele ya watoto chanzo mmomonyoko wa maadili

23 November 2023, 15:59

Na Hobokela Lwinga

Inaelezwa kuwa wazazi na walezi wamekuwa kichocheo kikubwa cha mmonyoko wa maadili hali inayosababisha uwepo wa matendo ya kikatili kwenye jamii.

Hayo yameelezwa na mkuu wa dawati la jinsia jeshi la polisi mkoa wa Mbeya Inspekta Loveness Mtemi wakati akizungumza na kituo hiki kuelekea katika kilele cha siku kumi na sita Novemba 25,2023.

Afande Loveness amesema wazazi na walezi wamejisahau kutoa malezi mazuri kwa kisingizio cha kuwa kwenye shughuli za kiuchumi.

Mkuu wa dawati la jinsia jeshi la polisi mkoa wa Mbeya Insipecta Loveness Mtemi(picha na Hobokela Lwinga)
Sauti ya Mkuu wa dawati la jinsia jeshi la polisi mkoa wa Mbeya Insipecta Loveness Mtemi 1

Aidha Amesema wazazi anapaswa kuwa karibu na watoto na kuzungumza nao juu ya maisha huku akisema wanaume wamekuwa waoga kutoa taarifa za ukatilii wanaofanyiwa na wake zao.

Sauti ya Mkuu wa dawati la jinsia jeshi la polisi mkoa wa Mbeya Insipecta Loveness Mtemi 2

Sambamba na hayo afande loveness Amesema changamoto kubwa kama dawati wanakumbana nazo ni ushirikiano mdogo wa watu waliofanyiwa ukatili pamoja wenye kesi kususia kesi yao.

Mkuu wa dawati la jinsia jeshi la polisi mkoa wa Mbeya Insipecta Loveness Mtemi(picha na Hobokela Lwinga)
Sauti ya Mkuu wa dawati la jinsia jeshi la polisi mkoa wa Mbeya Insipecta Loveness Mtemi 3

Maadhimisho ya kupinga siku kumi na sita za ukatili kitaifa zinatarajiwa kuzinduliwa Jumamosi novemba 25,2023 mkoani Geita na zinakwenda na kauli mbiu isemayo wekeza kuzuia ukatili wa kijinsia.

Ivillah Mgala mtangazaji baraka fm wakati akifanya mahojiano na Mkuu wa dawati la jinsia jeshi la polisi mkoa wa Mbeya Insipecta Loveness Mtemi(picha na Hobokela Lwinga)