Baraka FM

Ukatili wa kingono unakwamisha ndoto za wasichana wengi

11 October 2023, 19:23

Inspecta Loveness Mtemi mkuu wa dawati la polisi jinsia na watoto mkoa wa Mbeya(picha na Ezra mwilwa)

Mtoto wa kike amekuwa akikutana na changamoto nyingi tofauti na mtoto wa kiume na hii ndio sababu ya mtoto wa kike kulindwa na kupinga ukatili anaofanyiwa.

Na Ezra Mwilwa

Wazazi na walezi mkoani Mbeya wameshauriwa kumlinda mtoto wakike na kutoa taarifa za ukatili wa kijinsia wanao fanyiwa katika jamii zinazo wazunguka.

Wito huo umetolewa na inspecta Loveness Mtemi mkuu wa dawati la polisi jinsia na watoto mkoa wa mbeya wakati akizungumzia siku ya mtoto wa kike duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo October 11 ya kila mwaka.

Inspecta Loveness ameongeza kuwa ukatili wa kingono ambao watoto wakike wamekua wakifanyiwa unasababisha kushidwa kuhitimu masomo yao na kukatisha ndoto zao.

Sauti ya inspecta Loveness Mtemi mkuu wa dawati la polisi jinsia na watoto mkoa wa Mbeya

Mmoja ya wazazi jijini mbeya rehema kapoja amesema watoto wa kike wanahitaji kupewa haki sawa katika nyanja mbalimbali ikiwemo kulindwa ,kupata  elimu kuthaminiwa .

Naye mmoja wawasichana agness shayo amewaomba wazazi kuweza kuwasaidia watoto wakike kutimiza ndotozao kwakuwapa hitaji yao ya msingi pindi wawapo mashuleni na mazingirayao kwaujumla