Baraka FM

Mbeya UWSA yakabidhi bando 8 za mabati kwa shule na ofisi ya mtaa

23 March 2024, 07:20

Kaimu mkurugenzi Barnabas Konga (wa tatu kutoka kulia)akiwa na baadhi ya watendaji wa mamlaka wakati wa kukabidhi bati(picha na Ezekiel Kamanga)

Nyuma ya mafanikio yako wapo watu wanaokuwezesha hivyo tunapaswa kujifunza kuwa na shukrani,haya tunafundishwa na mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Mbeya ambao wameona umuhimu wa kurudi kwa jamii kwa kurudisha kwa jamii baadhi ya mafanikio yake.

Na Ezekiel Kamanga

Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mbeya (MBEYA – UWSA)imekabidhi bando tano za mabati kwa shule shule ya msingi Utengule Usongwe Mbeya Vijini na bando tano kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya mtaa wa Tonya Kata ya Ilomba Jjijini Mbeya.

Akikabidhi mabati hayo Kaimu Meneja Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Mbeya Mhandisi Barnabas Konga amesema ni sehemu ya maadhimisho ya kilele cha wiki ya maji sanjari na kurudisha fadhila kwenye jamii.

Diwani Yona Ntunjilwa Kata ya Utengule Usongwe amesema msaada uliotolewa utaleta chachu kwenye elimu na kuahidi kuulinda mradi wa maji Ilunga.

Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Tonya Kata ya Ilomba Eusebio Mihayo ameishuru Mamlaka kwa msaada huo na kuahidi kutoa ushirikiano hasa ulinzi wa vyanzo vya maji.

Diwani wa Kata ya Ilomba Tonebu Chaula mbsli ya kumpongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika utendaji kazi pia ameipongeza Mamlaka kwa namna inavyorudisha fadhila kwenye jamii.

Maadhimisho ya wiki ya maji yalianza machi 16,2024 na yametamatika machi 22,2024 kwa Mamlaka kutoa elimu kwa makundi mbalimbali,upandaji wa miti kwenye vyanzo vya maji,kutembelea miradi ya maji ukiwemo wa Kiwira,Mwasenkwa na Ilinga.