Baraka FM

Moravian Jimbo la Kusini yaendesha semina kwa watumishi wake

13 April 2024, 11:16

Wanasema elimu haina mwisho,unapopata fursa ya kupata elimu huna bidi kuikimbia na badala yake unapswa kuiwa mpokeaji ili kukuongezea ujuzi kwenye jambo unalolifanya au kulisimamia.

Na Mwandishi wetu

Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini limeendesha Semina ya pili kwa Viongozi wa Wilaya, Makatibu wa Idara na watendaji wa Taasisi zilizo chini ya Kanisa hilo.

Pamoja na mambo mengine, semina hiyo imegusia mambo mbalimbali ikiwemo Usimamizi wa mipango ya Kanisa, Usimamizi wa wakati na uhusiano katika utendaji wa kazi.

Semina hiyo iliyofunguliwa na Baba Askofu Kenan Salim Panja wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini, imefanyika tarehe 12/04/2024 ndani ya Ukumbi wa Mikutano Lutengano Wilayani Rungwe.

Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini Mch. Ezekiel Mwasamboma(aliyesimama)picha na mwandishi wetu
Sauti ya Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini Mch. Ezekiel Mwasamboma

Semina hii inayofadhiliwa na Shirika la Mission 21, imeongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini Mch. Ezekiel Mwasamboma huku mafunzo yakitolewa pia na Makamu Mwenyekiti Mch. Jairy Sengo pamoja na Katibu Mkuu Mch. Stephen Mwaipopo.

Sauti za baadhi ya washiriki