Baraka FM

Mch. Pangani: Mwombeeni Rais, dumisheni amani

2 January 2024, 18:10

Na Kelvin Lameck

Askofu Mteule ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini Magharibi Mchungaji Robert Pangani amewataka waumini na Watanzania kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kudumisha amani katika nchi.

Pangani ameyasema hayo katika ibada ya mwaka mpya iliyofanyika ushirika mpya wa Halengo Jijini Mbeya.

Katika hatua nyingine amewaonya Watanzania kuendelea kuienzi amani iliyoko nchini tofauti na nchi nyingine ambako milio ya bunduki imekuwa ni kitu cha kawaida.

Pangani ametumia nafasi hiyo kusoma neno kutoka kitabu cha Biblia ambalo ndilo msingi katika imani ya Kikristo.

Awali neno la utangulizi limesomwa na mchungaji wa ushirika Wilfred Ghambi.

Amani katika nchi ndiyo msingi wa maendeleo katika nchi yoyote pasipo na amani hata waumini hawawezi kupata muda wa kumwabudu Mungu.