Baraka FM

TMB yapiga marufuku wauzaji nyama kupuliza dawa yenye sumu buchani

28 March 2024, 20:15

Na mwandishi wetu

Bodi ya Nyama Tanzania (TMB) Nyanda za Juu Kusini imepiga marufuku wauzaji wa bucha za nyama kuachana na tabia ya kupuliza dawa zenye sumu ili kulinda afya za walaji.

Ofisa Mfawidhi wa Bodi ya Nyama Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Dkt. Mpoki Alinanuswe amesema jana mkoani hapa wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Ofisa Mfawidhi wa Bodi ya Nyama Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Dkt. Mpoki Alinanuswe

Amesema kitendo cha wauzaji kupuliza sumu kunaweza kuleta madhara makubwa kwa walaji huku akibainisha watu 10 wamechukuliwa hatua katika mikoa ya Mbeya na Songwe.