Baraka FM

St. Francis Mbeya wafanya maombi kabla ya mtihani kidato cha nne

13 November 2023, 15:48

Na Deus Mellah

Wakati mtihani wa taifa wa kidato cha nne ukianza leo  kwa shule zote za sekondari nchini  wanafunzi  kidato cha nne wa shule ya St. Francis girls ya jijini Mbeya wamefanya ibada  maalumu ya kumuomba Mungu ili aweze kuwasaidia kufanya vizuri katika mitihani hiyo.

Wakizungumza na kituo hiki katika ibada hiyo iliyofanyika katika kanisa la Moravian Tanzania jimbo la kusini  magharibi ushirika wa Ruanda wamesema mtihani wa taifa wa kidato cha nne ndio muongozo wa maisha yao hivyo ni jambo la msingi kumtegemea Mungu.

Mmoja wa wanafunzi hao Yunislois Spaika amesema kuwa wao kama wanafunzi wamejianda vizuri  katika mtihani huo  wa taifa wa kidato cha nne

sauti ya mwanafunzi Yunislois Spaika

Naye Faraja Chanila amewaomba wanafunzi wengine wanaofanya  mithani  leo kuendelea kumwamini na kumtegemea Mungu pekee katika mtihani  huo.

Baadhi ya wazazi na wanafunzi wakiwa kwenye maombi katika kanisa la Moravian jimbo la kusini magharibi ushirika wa Ruanda Mbeya(Picha na Deus Mellah)
sauti ya Faraja Chanila

Kwa upande wake mch Jamson Mwiligumo mwalimu wa shule ya St.Francis amewataka wanafunzi mbalimbali wanaofanya mitihani kuwa watulivu katika chumba cha mtihani.

Pia amewaomba wazazi  na walezi kuwa mstari wa mbele katika kuwaunga  mkono watoto wao wanaofanya mtihani ili waweze kutimiza ndoto zao za kielimu.

Mch Jamson Mwiligumo mwalimu wa shule ya St.Francis Sekondari Mbeya(Picha na Deus Mellah)

Ikumbuke kuwa mtihani wa taifa wa kidatio cha nne umeanza novemba 13,2023 katika shule zote za sekondari nchini.