Baraka FM

Rungwe kupokea vitambulisho vya taifa 69,638

5 December 2023, 14:58

Na mwandishi wetu 

Mkuu wa wilaya ya Rungwe Mhe. Jaffar Haniu amezindua zoezi la ugawaji wa vitambulisho vya  taifa (NIDA) leo tarehe 5.12.2023.

Zoezi limezinduliwa katika kata ya Kyimo tarafa ya Ukukwe.

 Mhe Haniu ameeleza kuwa jumla ya vitambulisho 69638 vitatolewa  kwa Wakazi wa wilaya ya Rungwe huku Kata ya Kyimo ikipokea jumla ya vitambulisho 2850.

Mhe Haniu amepongeza kwa hatua hii serikali imefanya na kuwa itarahisha utambulisho kwa wananchi katika kupata huduma mbalimbali.

Mkuu wa wilaya ya Rungwe Mhe. Jaffar Haniu(picha na mwandishi wetu)

Ameeleza kuwa uwepo wa kitambulisho kwa kila mkazi utasaidia kupata huduma mbalimbali hususani  Mbolea ,Kibenki, Vitambulisho vya bima ya  afya na hivyo kila mmoja hana budi kuvitunza kwani serikali imetumia gharama kubwa kuvitengene

Aidha Haniu amekemea vitendo vya kukaribisha wageni kutoka katika mataifa ya jirani bila kufuata taratibu na kuwa kufanya hivyo kunahatarisha usalama wa watu na mali zao

Pamoja na hayo ameagiza watendaji wote wanaofanikisha upatikanaji wa vitambulisho kutoandikisha watu kutoka mataifa ya jirani.

Wakati huo huo  mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Rungwe Mhe Mpokigwa Mwankuga amepongeza Serikali kwa kazi hiyo nzuri hatua itakayosaidia upatikanaji wa huduma mbalimbali kwa wananchi hasa katika msimu huu wa kilimo.