Baraka FM

Paradise Mission kuadhimisha miaka mitatu na Rais Samia

12 March 2024, 22:24

Mkurugenzi wa shule ya Paradise Mission Ndele Mwaselela (Picha Hobokela Lwinga)

Kila binadamu anayefanikiwa nyuma ya mafanikio yake lazima awepo mtu anayesukuma mafanikio hayo. Kutokana na hilo taasisi ya shule yenye mchepuo wa lugha ya kiingereza ya Paradise Mission imeona kwa miaka mitatu imefanikiwa kutoa elimu hasa kwa wakazi wa mkoa wa Mbeya na kuamua kuadhimisha pamoja na Rais Samia miaka mitatu tangu aingie madarakani.

Na Hobokela Lwinga

Shule ya mchepuo wa kiingereza Paradise Mission inayopatikana kata ya Nsalala halmashauri ya Mbeya inatarajia kuadhimisha miaka mitatu tangu kuanzishwa kwake kwa kurudisha shukrani kwa jamii kwa kutoa vitu mbalimbali ikiwemo kutoa vifaa vya shule kwa wanafunzi katika mkoa wa Mbeya.

Akizungumza na vyombo vya habari katika hoteli ya eden iliyopo jijini Mbeya mkurugenzi wa Paradise Missionndugu Ndele Mwaselela amesema kilele cha sherehe za miaka mitatu hiyo itafanyika machi 27 mwaka huu.

Sauti ya Mkurugenzi wa shule ya Paradise mission Ndele Mwaselela

Ndugu Mwaselela Amesema katika wiki hiyo yatafanyika matendo mbali mbali ikiwemo kutoa bima,kusomesha wanafunzi wasiojiweza pamoja na kutoa mahitaji ya shule.

Sauti ya Mkurugenzi wa shule ya Paradise mission Ndele Mwaselela

Sambamba na hayo amesema halmashauri zote zitafikiwa na Zaidi watalenga kuyafikia makundi yaliyopo pembezoni mwa miji.

Sauti ya Mkurugenzi wa shule ya Paradise mission Ndele Mwaselela