Baraka FM

Mchungaji kanisa la Moravian afariki Dunia

17 November 2023, 21:48

Picha ya marehemu mch.Sifael Mwashibanda

Na Hobokela Lwinga

Mchungaji wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini Magharibi ushirika wa Meta Mbeya Sifael Mwashibanda amefariki Dunia jijini Dar es salaam alikokuwa anapatiwa matibabu.

Akitoa taarifa ya kifo cha mch.Sifael Mwashibanda, Katibu mkuu wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi Ndugu Israeli Mwakilasa amesema mchungaji Mwashibanda amefariki usiku wa kuamkia Leo Tarehe 17/11/2023 jijini Dar es salaam ambako alikuwa anapatiwa matibabu ya Ugonjwa wa Salatani.

Katibu mkuu wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi Ndugu Israeli Mwakilasa(Picha na Hobokela Lwinga)

Mwili wa marehemu Mchungaji Mwashibanda unatarajiwa kusafirishwa leo jioni 17/11/2023 kuja Mbeya Ushirika wa Meta na unatarajiwa kufika kesho majira ya alfajiri.

Mazishi yanatarajiwa kufanyika kijiji cha Kalasha mji mdogo wa Mlowo wilaya ya Mbozi mkoani Songwe siku ya jumatatu tarehe 20/11/2023.

Ikumbukwe kuwa marehemu Mchungaji Mwashibanda amehudumu katika shirika mbalimbali na mpaka mauti inamfika alikuwa akihudumu ushirika wa Meta na mwalimu wa theologia chuo cha utengule

Bwana alitoa bwana ametwaa jina lake libarikiwe.