Baraka FM

Kayange: Viongozi wa maji wanaozuia wananchi kutoa kero wachukuliwe hatua

8 November 2023, 13:47

Mkurugenzi wa mamlaka hiyo CPA Gilbert Kayange akizungumza na wananchi mji mdogo wa mbalizi(picha na Sifael Kyonjola)

Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira jijini Mbeya imewaomba watumiaji wa maji kulipa ankara zao kwa wakati ili mamlaka hiyo iweze kujiendesha na kutoa huduma kwa ufanisi.

Na Sifael Kyonjola

Akizungumza na kituo hiki mkurugenzi wa mamlaka hiyo CPA Gilbert Kayange amesema kuwa mamlaka hiyo haitegemei ruzuku kutoka serikalini hivyo ni muhimu wananchi walipe malipo yao. 

sauti ya Mkurugenzi wa mamlaka hiyo CPA Gilbert Kayange kuhusu kuhusu ulipaji wa ankara

Ameongeza kuwa mamlaka ya maji imeanza kutoa mita za luku za maji kwa makampuni makubwa ili watumiaji walipe kulingana na matumizi yao huku akisisitiza kuwa mchakato huo utawafikia wananchi wote.

Baadhi ya akina mama wakifuatilia mkutano uliandaliwa na mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Mbeya (picha na Sifael Kyonjola)
Mkurugenzi wa mamlaka hiyo CPA Gilbert Kayange

Katika hatua nyingine amemtaka mkurugenzi wa maji katika mji wa Mbalizi  GEORGE ALBANO kuwachukulia hatua baadhi ya watumishi wanaozuia wananchi kufikisha kero zao kwa viongozi wa mamlaka hiyo ili hatua zichukuliwe

Wananchi mji mdogo wa Mbalizi Mbeya wakifuatilia mkutano ulihusisha mamlaka ya maji na usafi wa mazingira Mbeya