Baraka FM

Ziara ya RC Homera yawa lulu kwa wawekezaji, aahidi ushirikiano na serikali

18 January 2024, 20:36

Na Hobokela Lwinga

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Cde Juma Zuberi Homera amewahakikishia Usalama wa Kutosha Wafanyabiashara na wawekezaji wa Mkoa wa huo ili kuendelea kufanya Shughuli zao za Uzalishaji Mali wenye tija kwa Serikali na Wakazi wa Mbeya kwa Ujumla.

Ameyasema hayo leo January 17 2024 alipofanya Ziara ya Kutembelea na Kukagua Kiwanda Cha Uzalishaji Magodoro(Mbeya Foam) kilichopo Kata ya Iwambi Halmashauri ya Jiji la Mbeya.

Homera Amesema Mbeya inazidi kutanuka hasa katika miundombinu ya Vuwanda na Uwepo wa Mbeya Foam unazidi kuongeza Soko la Ajira hasa kwa Vijana.

Hata hivyo Homera ametoa Wito kwa Wakazi wa Mbeya na Nyanda za Juu Kusini kuzitumia Bidhaa za Mbeya Foam kwa kuwa Zina Ubora wa Kutosha.