Baraka FM

Naibu Waziri Mkuu awasili Mbeya kwa ziara ya siku mbili

20 February 2024, 10:42

Na Hobokela Lwinga

Naibu Waziri Mkuu na Waziri Wa Nishati Mh, Dkt. Dotto Biteko amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Songwe na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera tayari kwa kuanza ziara yake ya kikazi ya siku Mbili katika Wilaya za Rungwe, Mbeya na Mbarali.

Katika ziara hiyo Mh: Biteko atatembelea na kukagua Mradi wa Joto ARDHI (Geothermal) ulioko Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe na kisha atazindua Miradi ya Umeme Vijijini REA Wilayani Mbarali.

Hii ni kwa mara ya kwanza kwa Mh: Biteko kufika Mbeya tangu ateuliwe kuwa Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.