Baraka FM

Askofu Mwakanani: Mnapogombea zingatieni misingi na kanuni za uongozi

9 April 2024, 13:46

Askofu mkuu wa Makanisa ya Brotherhood Tanzania Rabby Mwakanani(kulia aliyevaa Joho)

Mwaka 2024 kunatarajia kuwa na uchaguzi wa serikali za mitaa nchi nzima huku ikitarajiwa kupatikana kwa wenyeviti wa mitaa na vijiji sambamba na 2025 kunatarajiwa kuwepo kwa uchaguzi mkuu wa Rais, Wabungeni na Madiwani.

Na Kelvin Lameck

Viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa wenye nia ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wametakiwa kuzingatia misingi na kanuni za uongozi.

Ushauri huo umetolewa na Askofu mkuu wa Makanisa ya Brotherhood Rabby Mwakanani wakati akizungumza na kituo hiki katika kuelekea uchaguzi utakaofanyika mwaka huu na mwakani.

Askofu Mwakanani amesema kuwa Misingi na kanuni hizo zitawasaidia wanasiasa waweze kufika mbali katika kutimiza malengo yao huku akiwataka waache kuonesha silaha zao mapema kwa lengo la kuepukana na vikwazo.

Sauti ya Askofu mkuu wa Makanisa ya Brotherhood Rabby Mwakanani

Katika hatua nyingine ameongeza kuwa wanasiasa wanapaswa kuepukana na makundi ndani ya chama au kwenye jamii kwani wanaweza kuwagawa watu jambo ambalo sio zuri.

Sauti ya Askofu mkuu wa Makanisa ya Brotherhood Rabby Mwakanani

Aidha amewasihi viongozi hao kuwa na Upendo, Umoja na Mshikamano huku wakimtanguliza Mungu katika mipango yao.