Baraka FM

Kamati zapongezwa utekelezaji wa miradi Rungwe

6 February 2024, 10:47

Na mwandishi wetu

Kamati ya fedha (FUM) imefanya ukaguzi wa ujenzi wa shule mpya ya Msingi Umoja yenye Mchepuo wa Kingereza iliyopo Ilenge kata ya KyimoMwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Rungwe Mheshimiwa Mpokigwa Mwankuga ndiye aliyeongoza kamati hii ambapo pamoja na mambo mengine amezipongeza kamati zote zilizotekeleza miradi huu kwa viwango na stahiki kwa kutolea huduma ya elimu.

Jumla ya vyumba vinne vya madarasa, ofisi pamoja na vyoo vya walimu na wanafunzi vimejengwa.

Gharama ya ujenzi wa shule hii umetokana na Mapato ya ndani ya Halmashauri.Shule tayari imefunguliwa na kuendelea kutoa huduma ya elimu