Baraka FM

Dr.Tulia:Toeni elimu huo ndio wajibu wenu kama ustawi wa jamii

14 November 2023, 19:45

Dr.Tulia Aksnon Mwansasu akizungumza na wataalamu wa ustawi wa jamii nchi katika ukumbi wa Tughimbe jijini Mbeya(picha na Deus Mellah)

Na Deus Mellah

Spika wa bunge la jamhuri wa muungano wa tanzania ambaye pia ni mbunge wa jimbo la mbeya mjini Dr Tulia Akson amewataka  mafiasa  ustawi wa jamii  nchini  kuendelea kutoa elimu  kwa jamii kuhusu masuala mbalimbali  yanayoihusu jamii hasa katika kuhakikisha jamii inakuwa na usawa.

Ameyasema hayo wakati wa  ufunguzi wa kongamono la  kitaaluma pamoja na mkutano wa mwaka wa wanataaluma ya ustawi wa jamii Tanzania   TASWO  linaloendelea katika  ukumbi wa tugimbe jijini mbeya.

Dr tulia amesema  maafisa  wanawajibu wa kuendelea kutoa elimu kwa jamii kwani bado elimu inahitajika  juu ya uelewa wa mambo na kufanya tafiti mbalimbali .

Maafisa ustawi wakishiriki mkutano maalumu katika ukumbi wa tughimbe jijini Mbeya(picha na Deus Mellah)
Sauti ya Spika wa bunge la jamhuri wa muungano wa tanzania ambaye pia ni mbunge wa jimbo la mbeya mjini Dr Tulia Akson

Naye  Salma Fundi ambaye ni makamu mwenyekiti wa TASWO  amesema  wao kama  wanaustawi wa jamii  watahakikisha wanaenda kuyafanyia kazi yale yote ambayo wameagizwa na spika.

Makamu mwenyekiti wa TASWO Salma Fundi
Sauti ya Naye  Salma Fundi makamu mwenyekiti wa TASWO

kwa upande wake afisa tawala wa mkoa wa mbeya Mohamed Fakili  amewataka maafisa ustawi wa jamii nchini kufanya kazi kwa weledi ili wawe mfano wa kuigwa katika jamii.

Sauti ya afisa tawala wa mkoa wa mbeya Mohamed Fakili 

Songoro Jumbe Msongo katibu mwenezi wa  wataaluma wa ustawi wa jamii Tanzania   amesema kuwa wataenda kufanya kazi  kwa weledi mkubwa ili jamii iwe yenye usawa.

Sauti ya Songoro Jumbe Msongo katibu mwenezi wa  wataaluma wa ustawi wa jamii Tanzania