Baraka FM

Serikali yawapa tabasamu wakazi wa kata ya Lupepo wilayani Rungwe

9 January 2024, 18:19

Na mwandishi wetu

Adha ya kutembea umbali mrefu kwa wanafunzi wa sekondari sasa imemalizika kwa wakazi wa kata ya Lupepo kufuatia kukamilika kwa ujenzi wa vyumba vya madarasa , Maabara, Maktaba, vyoo na jengo la Utawala katika shule Mpya ya Sekondari Lupepo

Hatua hii imefikiwa baada ya serikali kutoa kiasi cha Shilingi Million 583 kwa ajili ya ujenzi kwa kushirikisha nguvu za wananchi.

Shule hii inatarajiwa kuanza masomo yake januari 8, 2024 na imesajiliwa kwa namba S.6493.

Shule nyingine Mpya ya sekondari iliyosajiliwa ni pamoja na Isaka iliyopo kata ya Nkunga kwa usajili namba S.6491.

Shule hii ya Isaka iliyopo katika kijiji cha Isaka mita chache kutoka barabara ya Kiwira-Igogwe imekamilishwa kwa Mapato ya ndani ya Halmashauri pamoja na nguvu za wananchi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo.