Baraka FM

TARI yatoa elimu ya kilimo biashara kwa wakulima mikoa ya Nyanda za Juu Kusini

11 September 2023, 16:22

Sehemu ya uzalishaji wa mbegu za mfano katika kituo cha utafiti wa kilimo TARI Uyole Mbeya. Picha na Hobokela lwinga

Matumizi ya teknolojia yanatajwa kuwa kichocheo kikubwa katika kufanikisha sekta ya kilimo nchini.

Na Hobokela lwinga

Wakulima katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini wametakiwa kufuatilia elimu ya kilimo inayotolewa kupitia kwa wataalam wa kilimo na kujifunza uzalishaji bora wa mazao kwa kutumia vizuri teknolojia mbalimbali za kilimo  ili kuweza kuzalisha kwa tija na kupata faida kiuchumi.

Wito huo umetolewa na katibu tawala msaidizi na msimamiz wa uchumi na uzalishaji ofisi ya mkoa wa Mbeya Said Juma Madito akiwa mgeni rasmi katika maonesho ya kilimo biashara yaliyofanyika pembezoni mwa mashamba ya taasisi ya kilimo yaliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI UYOLE) inayopatikana halmashauri ya jiji la Mbeya.

Madito Amesema sekta ya kilimo imekuwa na changamoto mbalimbali hasa kwa wakulima wadogo ikiwemo upimaji wa afya ya udongo na gharama ya pembejeo.

Sauti ya katibu tawala msaidizi na msimamizi wa uchumi na uzalishaji ofisi ya mkoa wa Mbeya Said Juma Madito.

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa TARI Uyole Dkt. Denis Tipe Amesema lengo la maonesho hayo ya kilimo biashara ni kuwawezesha wakulima kujifunza teknoloji mbalimbali za kilimo zitakazowarahisishia kuzalisha kwa tija.

Sauti ya Dkt. Denis Tipe mkrugenzi TARI Nyanda za Juu Kusini.

Aidha katika maonesho hayo yamekuwepo maonesho ya mifugo yanayosimamiwa na  mkurugenzi wa taasisi ya utafiti wa mifugo Nyanda za Juu Kusini Edwin Chang’a ambaye amesema taasisi yake inajihusisha na utafiti wa ng’ombe wa maziwa na wanyama wasiocheua huku akiwataka wafugaji kufika kwenye kituo hicho ili kujipatia mbegu za uzalishaji wa chakula cha mifugo.

 Mkurugenzi wa taasisi ya utafiti wa mifugo Nyanda za Juu Kusini TARILI Edwin Chang’a.

Baadhi ya washiriki katika maonesho hayo wameishukru taasisi ya TARI Uyole kwa kuwezesha wakulima wananufaika na elimu inayotolewa na wataalam wa kilimo. 

Kauli mbiu ya maonesho ya kilimo biashara kwa 2023 ni kilimo biashara, tumia teknolojia bora na pembejeo sahihi ili kuongeza tija, uhakika wa chakula, lishe kipato, ajira na kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi .