Baraka FM

LHRC yatembelea kituo cha redio Baraka Jijini Mbeya

22 February 2024, 15:09

Na Hobokela Lwinga

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dkt. Anna Henga ametembelea Radio Baraka Fm iliyopo jiijini Mbeya.Dkt.

Henga amepata wasaa wa kujifunza namna ambavyo kituo hicho kinavyoendesha shughuli zake za kuwapatia elimu wasikilizaji wao hasa ya sheria na masuala ya Haki za Binadamu.

Hata hivyo meneja Baraka fm radio ndg. Charles Amlike ameomba taasisi zingine binafsi na Serikali kutembelea kituo na kujifunza mambo mbalimbali redioni hapo.

Baraka Fm ni miongoni mwa Radio jamii ambazo zimekuwa zikifanya kazi kwa ukaribu na LHRC hasa katika kuwafikishia Elimu ya Haki za Binadamu wananchi wa Mbeya na mikoa jirani inayojumuisha nyanda za juu kusini.