Baraka FM

Umuhimu wa kutunza macho yako ukiwa kazini

3 October 2023, 19:09

Daktari wa macho kutoka hospitali ya kanda ya Rufaa Mbeya daktari Khikasy Digna wakati akizungumza na kituo hiki kuelekea siku ya uoni wa macho duniani aliyepo kulia.(picha na Mpoki Japheth)

Katika maisha yetu ya kila siku tunashauriwa kutunza macho yetu kwa kupunguza matumizi ya simu pamoja na komputa hasa ukiwa kazini.

Na Mpoki Japheth

Wananchi mkoani Mbeya wameshauriwa kutunza macho yao ili kuepukana na changamoto ya tatizo la uoni hafifu.

Hayo yamesemwa na mtaalam wa macho kutoka hospitali ya kanda ya Rufaa Mbeya Dkt. Khikasy Digna wakati akizungumza na kituo hiki kuelekea siku ya uoni wa macho duniani itakayofanyika Oktoba 12 mwaka huu.

Daktari Digna amesema ni wajibu wa kila mtu kutunza macho yake kwani itamsaidia kulinda na kuepukana na matatizo mbalimbali.

Sauti ya daktari wa macho kutoka hospitali ya kanda ya Rufaa Mbeya Khikasy Digina

Aidha ameongeza kuwa katika kuelekea katika siku ya uoni wa macho duniani  watatoa elimu katika shule mbalimbali za msingi na sekondari. 

Sauti ya daktari wa macho kutoka hospitali ya kanda ya Rufaa Mbeya Khikasy Digna

Kwa upande wake daktari Judith Adonis amesema inatakiwa kujiwekea utaratibu wa kupima afya ya macho mara kwa mara ili kubaini mapema kama una tatizo na kupatiwa matibabu.

Sauti ya muuguzi kutoka hospitali ya kanda ya Rufaa Mbeya Judith Adonis