Baraka FM

Bi. Mdidi: Epukeni rushwa, fuateni sheria za utumishi wa umma

1 February 2024, 09:06

Na mwandishi wetu

Kaimu Mweka hazina Halmashauri ya wilaya ya Rungwe Bi. Kijakazi Mdidi ameongoza kikao cha watumishi wapya (Ajira ya Mkataba) katika sekta ya mapato lengo likiwa ni kuwajengea uwezo sambamba na kuwapa maelekezo dhidi ya namna bora ya kukusanya mapato.

Bi Mdidi amewakumbusha watumishi hawa kuhakikisha wanafuata Sheria , Taratibu na Kanuni za utumishi wa umma hii ikiwa ni pamoja kuepukana na vitendo vya rushwa ikiwa ni nyenzo muhimu ya utendaji haki katika jamii na kuongeza mapato ya serikali.

Amesema kila mtumishi lazima ahakikishe mapato ya serikali yanaongezeka kwa kasi na kuhakikisha anafanya kazi kwa bidii usiku na mchana.

Aidha wamekumbushwa kuhakikisha wanatunza na kutochezea vitendea kazi watakavyopewa ikiwemo machine ya kukusanyia mapato (POS) ili kuleta ufanisi katika ukusanyaji mapato.

Jumla ya Watumishi 16 wamechaguliwa baada ya kushinda usaili uliofanyika tarehe 19.01.2024.