Baraka FM

Mkuu wa mkoa wa Songwe amezindua zoezi la ugawaji miche TACRI

19 December 2023, 20:22

Na mwandishi wetu

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Dkt. Francis K. Michael, amezindua zoezi la ugawaji miche ya Kahawa, miti ya Mbao, matunda na vivuli zaidi ya Million sita na kusisitiza jamii kuhamasika kupanda miti kwa wingi kwa faida yao na Taifa kwa ujumla.

Mhe Dkt. Francis, amesema hayo wakati akizungumza kwenye uzinduzi mpango huo katika Ofisi ya Taasisi ya Utafiti wa zao la Kahawa TACRI Kanda ya Nyanda za Juu Kusini (Mbeya, Songwe na Rukwa) kilichopo Mbimba Vwawa Mbozi.

Amekipongeza kituo cha utafiti TACRI kwa ubunifu wa mbegu mbalimbali za miti katika kusaidia kuongeza uzalishaji wa mazao na miti mingine rafiki kwa mazingira ili kulinda uoto wa asili ambapo pia ameiasa jamii kila mmoja kuhamasika kupanda miti kwenye eneo lake ili kutunza mazingira.