Baraka FM

Wanahabari wajengewa uwezo matumizi takwimu za sensa ya watu, makazi

29 January 2024, 18:09

Na Hobokela Lwinga

Kamisaa wa Sensa nchini Anne Makinda amesisitiza waandishi wa habari kutumia matokeo ya takwimu za sensa ya watu na makazi kwa usahihi ili kuandika habari zenye ubora na usahihi zitakazosaidia katika kuleta maendeleo kwa wananchi.

Makinda ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa semina ya Uwasilishaji, Usambazaji na Uhamasishaji wa matumizi ya sensa ya watu na makazi ya 2022 kwa waandishi wa habari wa Mikoa ya Mbeya, Iringa na Songwe.

Sauti ya Kamisaa wa Sensa nchini Anne Makinda

Aidha Meneja takwimu mkoa wa Mbeya John Lyakurwa ameeleza lengo la kutoa mafunzo hayo huku mkuu wa wilaya ya mbeya Beno malisa amewaomba waandishi wa habari kutumia taalima zao kwa weledi ili ziweze kuwasaidia wananchi.

Sauti ya Meneja takwimu mkoa wa Mbeya John Lyakurwa na mkuu wa wilaya ya mbeya Beno malisa

Kwa upande wao waandishi wa habari walioshiriki mafunzo hayo wamesema yatawasidia katika kazi zao za uandishi wa habari.

Sauti za baadhi ya waandishi wa habari walioshiriki mafunzo