Baraka FM

Bei za mafuta zasababisha mgomo wa daladala Mbeya, nauli zapandishwa kiholela

11 October 2023, 14:19

Baadhi ya gari zikiwa hazifanyi kazi eneo la standi ya Kabwe jijini Mbeya.

Wakazi wa Mbeya wamejikuta wakiamka na kukuta wanakosa usafiri wa kwenda kwenye shughuli zao hali iliyowasababishia kutumia usafiri wa bajaji kwa gharama kubwa.

Na Ezra Mwilwa

Wananchi jijini Mbeya wameiomba Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini LATRA kuchukua hatua za kisheria kwa madereva wa gari za abiria zinazofanya safari za Mbeya mjini hadi Mbalizi kutokana na kupandisha nauli kiholela.

Wakizungumza na kituo hiki wananchi hao wamedai kuwa hatua hiyo inawasababishia usumbufu wanapokuwa safarini kwani wanatozwa shilingi mia saba kati ya kituo na kituo badala ya shilingi mia tano.

Sauti ya baadhi ya abiria jijini Mbeya

Kwa upande wao baadhi ya madereva wamesema kuwa wamefikia hatua hiyo kutokana na kupanda kwa gharama za mafuta ili kuwarahisishia gharama za uendeshaji.

Picha ya baadhi ya gari za daladala zikiwa zimepakiwa kushinikiza upandaji wa nauli katika mji mdogo wa Mbalizi Mbeya (Picha na Ezra Mwiliwe)
Sauti ya baadhi ya madereva wa jiji la Mbeya

Naye meneja wa LATRA Mbeya Omary Ayubu amesema mpaka sasa hakuna viwango vipya vya nauli walivyotangaza hivyo amewataka madereva kusubiri taarifa ya serikali kuhusu viwango vipya vya nauli badala ya kupandisha kiholela.

Sauti ya meneja wa mamlaka ya udhibiti usafiri ardhini LATRA Mbeya Omary Ayubu