Baraka FM

Zaidi ya wanafunzi wa kike 130 wapatiwa taulo za kike Yalawe sekondari Mbeya Dc

26 October 2023, 13:40

Picha ya pamoja kati ya waratibu wa tukio walimu na wanafuynzi (picha na Hobokela Lwinga)

Mtoto wa kike amekuwa akipitia madhira kadhaa ambazo zimekuwa zikimfanya kukosa masomo,wengine kutokana na ugumu wa maisha waliyonayo wazazi wao wamekuwa wakiacha shule na kujikuta wakishindwa kutimiza ndoto zao,hali hiyo imekuwa ikichochea uwepo wa ndoa za utotoni.

Na Hobokela Lwinga

Zaidi ya wanafunzi wa kike 130 katika shule ya sekondari yalawe inayopatikana kata ya santilya halmashauri ya mbeya wamepatiwa  msaada wa taulo za kike uliotolewa na kituo cha radio Baraka.

Akizungumza na kwa niaba ya kituo  cha radio Baraka wakati wa kukabidhi msaada huo ulioratibiwa na kipindi cha radio cha kivulini,meneja wa vipindi Mpoki Japhet amesema kituo hicho kimekuwa na utaratibu wa kurudisha shukrani kwa jamii kwa kutoa msaada  kwenye makundi mbalimbali yenye uhitaji.

meneja wa vipindi Mpoki Japhet (Picha na Hobokela Lwinga)
Sauti ya meneja wa vipindi Baraka fm Mpoki Japhet

Kwa upande wake mwalimu Betina Kyando katika shule hiyo amesema msaada huo utapunguza changamoto ya wanafunzi wengi wa kike ambao walikuwa wanakosa masomo kwa takribani siku kuanzia tano kipindi cha hedhi zao.

Mwalimu Betina Kyando akizungumza baada ya kupokea msaada wa taulo za kike kwa wanafunzi wa Yalawe sekondari
Sauti ya mwalimu Betina Kyando

Aidha baadhi ya wanafunzi ambao wamenufaika na msaada huo wameishukru Baraka fm kwa kuwakumbuka na kuwaona  licha ya kuwa wapo kijijini  huku wakiomba wadau wengine kujitokeza kuwasaidia kutatua changamoto anazokumbana nazo motto wa kike.

Mtangazaji wa Baraka fm Anna Mbwilo(mratibu wa tukio) akitoa elimu ya matumizi ya taulo za kike kwa wanafunzi wa kikie Yalawe sekondari(picha na Hobokela Lwinga)
Sauti za wanafunzi Yalawe sekondari

Msaada huo umetolewa na kituo hicho kutokana na changamoto ambayo mtoto wa kike amekuwa akikumbana nayo hasa akiwa kwenye siku zake.

mtangazaji wa Baraka fm Ivillah Mgalla akikabidhi taulo kwa mwanafunzi Yalawe sekondari(picha na Hobokela Lwinga)