Baraka FM

10 wakamatwa wakitorosha kilo 9.8 za dhahabu mkoani Mbeya

19 March 2024, 18:42

Hizi baadhi tu ya dhahabu ambazo zimekamatwa (picha na Hobokela Lwinga)

Shughuli za kila mwanadamu zinatengemea kufanywa kupitia taratibu na sheria za nchi,na endapo mtu akikiuka hayo ni lazima achukuliwe hatua kwa mujibu wa taratibu na sheria za nchi.

Na Hobokela Lwinga

Watu 10 wanashikiliwa na jeshi la polisi Mkoani Mbeya kwa tuhuma za kutorosha vipande 334 vya dhabu iliyochomwa yenye uzito wa kilogramu 9.5 ambayo inaghalimu kiasi Cha fedha za kitanzania zaidi ya shilingi bilioni moja.

Akitoa taarifa kwa wanahabari jijini mbeya waziri wa madini Anthony Mavunde amesema watuhumiwa hao walikamwatwa machi 16 mwaka huu mtaa wa Ilomba na kata ya ilomba jijini mbeya wakiwa na vifaa vya kuchomea dhahabu na mizani ya kupimia pamoja na Sawa za kusafishia ambapo uchunguzi ukikamilika watafikishwa mahakamani.

Mavunde amesema tukio hili ni la pili kutokea Mkoani Mbeya na kuagiza kamishina wa madini kuzifuta leseni zote zinazomilikwa na watu hao pamoja na leseni zote zinazomilikea na watu hao nje ya Mkoa wa Mbeya.

Waziri wa madini Mhe.Anthony Mavunde(Picha na Hobokela Lwinga)
Sauti ya Waziri wa madini Mhe.Anthony Mavunde

Kwa upande wake mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mrakibu mwandamizi wa uhamiaji Mbarack Alhaji Batenga ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Chunya amesema ili kukomesha uhalifu unaofanywa na baadhi ya watu kwenye mitaa viongozi wa mitaa

Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mbarack Alhaji Batenga(katikati)akiwa ameshika bakuli lililo tumika kuhifadhia dhahabu(picha na Hobokela Lwinga)
Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mbarack Alhaji Batenga

Hata hivyo Kamanda wa Polisi ACP Benjamini Kuzaga amesema wao kama jeshi la polisi wataendelea kukabiliana na wahalifu wote wanaokiuka taratibu na sheria za nchi.

Katibu tawala mkoa wa Mbeya Rodrick Mpogole (kushoto)katika picha ya pamoja na kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya ACP Benjamin Kuzaga(kulia),picha na Hobokela Lwinga
Sauti ya kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya ACP Benjamin Kuzaga