Baraka FM

Mwananchi asombwa na maji Songwe, mwili haujulikani ulipo

23 January 2024, 18:19

Kanary Jaribu Haonga mhanga aliye sombwa na maji mto Mlowo mkoani Songwe

Na Deus Mellah

Mtu mmoja anayejulikana kwa jina la Kanary Jaribu Haonga mwenye umri wa miaka 26 mkazi wa kitongoji cha Iwagamoyo kata Itumpi mkoani Songwe amesombwa na maji wakati akijaribu kuvuka mto Mlowo eneo la kijiji cha Iyenga ni siku saba sasa mpaka leo hajapatikana hali iliyozua hofu kubwa kwa wananchi wa eneo hilo.

wakizungumza na kituo hiki ndugu wa kijana huyo wamesema kuwa wamefanya kila jitihada kwa kushirikiana na wananchi wa vijiji vya Itumpi na Iyenga kuutafuta mwili wa kijana huyo lakini mpaka sasa haujapatikana.

Akizungumza na kituo hiki dada wa kijana huyo Samehe Jaribu Haonga ameiomba jamii na watanzania kwa ujumla kopote watakapouona mwili huo wa mpendwa kutoa taarifa ili waweze kuupumnzisha mahali salama .

sauti ya Dada wa mhanga huyo Samehe Haonga

Diwani wa kata hiyo Samson Nzunda amekiri kutokea kwa tukio hilo katika kata yake huku akisema jitihada kubwa zimefanyika za kuhakikisha mwili wa kijana huyo unapatikana lakini zimegoonga mwamba laniki wanaendelea kuutafuta mwili wa kijana huyo.

sauti ya Diwani Samson Nzunda

Pia Ametoa Wito Kwa Jamii Katika Kipindi Hiki Ambacho Mvua Zinaendelea Kunyesha Maeneo Mbalimbali Kuacha Mazoea Ya UzoEfu Wa Kuvuka Maji Na Kuchukua Tahadhari Ili Kuweza Kuepukana Na Changamoto Inayoweza Kujitokeza.