Baraka FM

Wakristo watakiwa kuzalisha mali ili kujiongezea uchumi kwenye familia zao na kanisa

14 November 2023, 19:30

Na Hobokela Lwinga

Wakristo wametakiwa kuwa mstari wa mbele katika uzalishaji mali ili kuweza kuwa mfano na ushuhuda juu ya Mungu wanayemtumikia.

Wito huo umetolewa na katibu wa idara ya uwakili kanisa la Moravian Tanzania jimbo la kusini Magharibi Mch. Paul Mwambalaswa wakati akihubiri na kufundisha somo la kilimo katika ushirika wa Igodima jijini Mbeya.

Katibu wa idara ya uwakili kanisa la Moravian Tanzania jimbo la kusini Magharibi Mch. Paul Mwambalaswa(picha na Hobokela Lwinga)
Sauti ya katibu wa idara ya uwakili kanisa la Moravian Tanzania jimbo la kusini Magharibi Mch. Paul Mwambalaswa

Kwa upande wake Mch.Gama Simbowe amewakumbusha waumini wa ushirika wa Igodima kuendelea kumtolea Mungu sadaka katika kujenga hekalu la kuabudia.

Mchungaji wa ushirika wa Igodima Ezekia Fungo amesema masomo hayo yatawanufaisha waumini kukua kiuchumi na kanisa kwa ujumla.

Mchungaji wa ushirika wa Igodima Ezekia Fungo(picha na Hobokela Lwinga)
Sauti ya Mchungaji wa ushirika wa Igodima Ezekia Fungo