Baraka FM

Zahanati ya Ilenge  kata ya Kyimo wilayani Rungwe imefunguliwa

28 December 2023, 18:09

Na mwandishi wetu

Huduma ya Matibabu kwa Wagonjwa katika Zahanati ya Ilenge  kata ya Kyimo imefunguliwa leo rasmi tarehe 27.12.2023 na kutoa huduma mbalimbali kwa ikiwemo ya mama na mtoto.

Amesema pamoja na huduma zingine, wagonjwa wameendelea kunufaika na huduma ya Mama na Mtoto na Chanjo mbalimbali.

Zahanati ya Ilenge imejengwa na Serikali kwa Kushirikiana na Wananchi ambapo pamoja na Mfuko wa Jimbo pia Serikali imetoa kiasi cha Shilingi million 50 kwa ajili ya Ukamilishaji

Hata hivyo wananchi wameishukru serikali kwa kuhakikisha zahanati hiyo inaanza kutoa huduma hali itakayosababisha kupata matibabu kwa urahisi na kwa haraka.