Baraka FM

Wakristo wahimizwa kumtegemea Mungu kwenye maisha yao

29 March 2024, 12:43

Baadhi ya waumini kanisa la Moravian, ushirika wa Nzovwe(Picha na Rukia Chasanika).

Ijumaa Kuu kwa mkristo Ina nafasi kubwa kwani ni siku ambayo inatajwa kwenye Maandiko Matakatifu kuwa ndiyo ulimwengu ulipata wokovu na kibiblia kama mateso ya Yesu Kristo, kabla ya ufufuo wake wa siku Tatu.

Na Rukia Chasanika

Wakristo nchini wameshauriwa kumtegemea Mungu wanapopita katika changamoto mbalimbali za maisha.

Hayo yamesemwa na Mwinjilisti Suleiman Shani wakati akihubiri katika ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika katika kanisa la Moraviani Tanzania Jimbo la kusini magharibi ushirika wa Nzovwe mkoani Mbeya.

Mwinjilisti Shani amesema watu wanakataa tamaa kwa sababu hawamtegemei Mungu katika maisha yao ya ukristo.

Aidha ameongeza kuwa watu wanashindwa kufanikiwa kwa sababu wanafanya matendo mabaya ambayo kwa Mungu ni chukizo.

Mwinjilisti Suleiman Shani(picha na Rukia Chasanika)

Kwa upande wake mchungaji wa ushirika wa Moravian Nzovwe Jonam Msangawale amesema wanapokumbuka kufa na kufufuka kwa Bwana Yesu kila mkristo anapaswa kutubu dhambi na kuanza maisha mapya ya kumpendeza Mungu.

Mchungaji wa ushirika wa Moravian Nzovwe Jonam Msangawale (picha na Rukia Chasanika).

Baadhi ya waumini waliohudhuria ibada hiyo wamesema wamejifunza namna ya kuukulia wokovu na kutokataa tamaa maana Yesu alikufa kwa ajili yao.