Baraka FM

Wizara ya Maji yaishukru UNICEF

31 January 2024, 08:39

Na Ezekiel Kamanga

Naibu Waziri wa Maji Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) amefanya mazungumzo na Mwakilishi Mkazi mpya wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Wanawake na Watoto Duniani (UNICEF) nchini Tanzania Bi. Elke Wisch.

Mazungumzo yamefanyika katika ofisi za Wizara mji wa serikali wa Mtumba jijini Dodoma ambapo Bi. Elke amefika kujitambulisha. Mhe. Mahundi amewashukuru UNICEF kwa mchango wao katika sekta ya maji na kuwakaribisha katika kuwekeza zaidi.

Pia kushirikiana katika kutekeleza Program ya Maendeleo yaSekta ya Maji Awamu ya Tatu.

Kwa upande wake Bi. Elke amepongeza kwa ushirikiano wa muda mrefu kati ya Wizara ya Maji na UNICEF na ameahidi kuongeza ushirikiano na uwekezaji katika sekta ya maji hususani maeneo ya usafi wa mazingira, magonjwa ya mlipuko kwa jamii na kujenga uwezo katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.