Baraka FM

Toeni ushirikiano watoto wapate chanjo ya polio

18 September 2023, 20:14

waumini wa kanisa la Moraviani ushirika wa Shewa Mbeya wakifuatilia ibada mwishoni mwa wiki(picha na Hobokela Lwinga)

Msingi wa binadamu ni afya na unapo kuwa na afya ni lazima uilinde,katika maisha ya binadamu yeyote wakati anazaliwa ni lazima apewe ulinzi wa afya yake kwa kupatiwa chanjo ya magonjwa mbalimbali,hivi karibuni serikali imekuwa na msisitizo wa kila mtanzania kupata chanjo zikiwezo za uviko 19.kwasasa kampeni iliyoandaliwa inawahusu watoto wenye umri chini ya miaka 8 mzazi hakikisha mwanao hapitwi na chanjo hii kwani itamkinga dhidi ya ugonjwa wa polio unaotajwa kutokuwa na tiba endapo utaupata.

Na Hobokela Lwinga

Mkuu wa wilaya ya Mbeya Beno malisa amewataka wananchi wilayani kwake kushiriki vyema zoezi la chanjo ya polio kwa kuhakikisha watoto wao wanapata chanjo hiyo.

Hayo ameyazungumza wakati alipohudhuria ibada katika kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi ushirika wa shewa uliopo jijini Mbeya ambapo amesema zoezi hilo litaanza September 21 na kuhitimishwa September 24 mwaka huu.

mhe.Malisa Amesema zoezi kila mzazi mwenye mtoto kuanzia miaka nane anapaswa kuhakikisha anampeleka kwenye maeneo yaliyotengwa ili aweze kupatiwa matone ya chanjo ya polio.

Mkuu wa wilaya ya mbeya mhe.beno malisa akizungumza na waumini wa kanisa la Moravian ushirika wa Shewa Mbeya juu ya umuhimu wa chanjo ya polio(picha na Hobokela Lwinga)
sauti ya mkuu wa wilaya ya Mbeya akizungumzza katika ibada katika kanisa la Moravian shewa Mbeya

Baadhi ya waumini wa kanisa hilo wamesema wako tayari kutoa ushirikiano kwa kuwapeleka watoto wao kuwenda kupata chanjo lengo likiwa ni kuuiunga serikali mkono katika zoezi hilo.

waumini wa kanisa la Moravian Shewawakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Mbeya Beno Malisa katika ibada iliyofanyika mwishoni mwa wiki(picha na Hobokela Lwinga)