Baraka FM

Askofu Pangani: Kuweni waadilifu msimwangushe Rais

31 January 2024, 09:54

Askofu mteule mchungaji Robert Yondam Pangani(picha na Hobokela Lwinga)

Na Hobokela Lwinga
Viongozi waliopo kwenye taasisi za umma wametakiwa kuwa waaminifu na waadilifu katika utekelezaji wa majukumu yao ili kutokumuuangusha mheshimiwa Rais katika mipango yake ya kuongoza nchi.

Wito huo umetolewa na Askofu mteule mchungaji Robert Yondam Pangani wakati akihitimisha semina ya siku 43 katika kanisa la Moravian ushirika wa Yeriko uliopo mji mdogo wa Mbalizi mkoani Mbeya.

Katika hatua nyingine amewataka Wananchi kuwa walipa kodi kwani kufanya hivyo ni kutimiza adhima ya Mungu kwenye maandiko matakatifu sambamba na kuiombea nchi iendelee kuwa na amani.

Askofu mteule mchungaji Robert Yondam Pangani akiongoza maombi ya kuliombea Taifa(picha na Hobokela Lwinga)
Sauti ya Askofu mteule mchungaji Robert Yondam Pangani.

Awali mchungaji wa ushirika wa Yeriko Paul Mwampamba amesema semina hiyo imekuwa na mwendelezo wa kuombea taifa kutokana na Mambo mbalimbali ikiwemo kukomesha masuala ya Ukatili wa kijinsia.

Mchungaji wa ushirika wa Yeriko Paul Mwampamba akifurahia Jambo baada ya kupewa zawadi na Serikali ya mji mdogo wa Mbalizi (picha na Hobokela Lwinga)
Sauti ya Mchungaji wa ushirika wa Yeriko Paul Mwampamba

Hata hivyo akiwasilisha salamu za serikali diwani wa kata ya utengule usongwe Yona Ntunjilwa Amelishukru Kanisa kwa ushirikiano wanaoutoa kwa Serikali katika kuliombea taifa na kumuombea Rais samia huku akiwaomba waumini kuombea taifa ili amani iendelee kudumu ikiwa ni sambamba na kuombea uchaguzi wa serikali za mitaa.

Hawa ni baadhi ya waumini wa kanisa la Moravian Tanzania ushirika wa Yeriko Mbalizi (Picha na Hobokela Lwinga)
Sauti ya diwani wa kata ya utengule usongwe Yona Ntunjilwa

Kwa upande wake mwenyekiti wa kanisa la moravian wilaya ya Mbalizi Mch.Erica Samwanijembe amesema semina hiyo iwe chachu kwa wachungaji na waumini kumtafuta Mungu

Mwenyekiti wa kanisa la moravian Mch.Erica Samwanijembe(picha na Hobokela Lwinga)
Sauti ya mwenyekiti wa kanisa la moravian wilaya ya Mbalizi Mch.Erica Samwanijembe