Baraka FM

Mbeya yatia saini mikataba ya upimaji na PEPMIS

6 January 2024, 00:54

Na Hobokela Lwinga

Zoezi la Utiaji Saini wa Mikataba ya Mfumo MPYA wa Upimaji wa Utendaji Kazi wa Watumishi(PEPMIS) katika Mkoa wa Mbeya limefanyika ambapo limemhusisha Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya Rodrick Mpogolo na Wakurugenzi wa Halmashauri zote za Mkoa wa Mbeya kwaajiri ya Kwenda Kufanya Kazi ipasavyo katika vituo vyao.

Zoezi la Utiaji Saini limefanyika Leo Ijumaa January 05 2023 Katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Kuhudhuliwa na Washiriki Mbali mbali Wakiwemo Makatibu Tawala Wilaya, Wakurugenzi na Wataalamu kutoka Halmashauri za Mkoa wa Mbeya.

Ikumbukwe Wiki Kadhaa Nyuma Zoezi la Uingizwaji wa Taarifa za Watumishi katika Mfumo ulifanyika ambapo Leo Umehitimishwa na kuambatanisha Zoezi hilo la Utiaji Saini Mikataba ya PEPMIS.