Baraka FM

Mvua yakata mawasiliano ya miundombinu ya barabara Rungwe, Mbeya

17 April 2024, 12:12

Miundombinu kata ya Kapugi baada ya mvua kukata mawasiliano (Picha na Ezra Mwilwa)

Katika hali isiyotarajiwa wakazi wa kata ya Kapugi na Lyenje wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya wamekutana na adha ya kuharibika kwa miundombinu ya barabara iliyokuwa ikiwaunganisha na kusababisha shughuli mbalimbali za kiuchumi kusimama.

Na Ezra Mwilwa

Mvua zinazoendelea kunyesha zimesababisha barabara ya Kapugi-Lyenje Ikuti  kupitia mto Kiwira kuharibika  na hivyo kuondoa mawasiliano kati ya vijiji hivi viwili.

Mbunge wa jimbo la Rungwe Mhe. Anton Mwantona amefika katika eneo la tukio  na kukagua madhara yaliyojitokeza na amewaomba wakazi wa wilaya ya Rungwe kuendelea kuchukua tahadhari dhidi majanga katika kipindi hiki ambacho mvua zinaendelea kunyesha nchi nzima.

Mbunge Mwantona amewataka wananchi wa vijiji hivyo kuwa watulivu kwenye kipindi hiki kigumu kwani Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan atafanya kama alivyowapa barabara mwanzoni waamini hata sasa hawezi kuwsacha wapate shida kwa sababu anawapenda wananchi wa Kapugi, Lyenje na Ikuti.

Mbunge wa jimbo la Rungwe akiwa katika eneo la tukio(picha na Ezra Mwilwa)
Sauti ya Mbunge wa jimbo la Rungwe Mhe. Anton Mwantona

Naye Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Rungwe komrade Mwakipunga amefika katika eneo la tukio  na kuwapa pole wananchi wa kata Kapugi na Lyenje kwa kuharibikiwa na miundombinu ya barabara hiyo.

Kulia Mwenyekiti wa Ccm wilaya ya Rungwe(picha na Ezra Mwilwa)
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Rungwe komrade Mwakipunga

Nao baadhi ya wananchi wa vijiji hivyo wakiongozwa na Diwani wao Mhe. Abraham Kapange wamemshukuru Mbunge na chama kwa kufika katika eneo la tukio na kuwafariji.

Baadhi ya wananchi wakiwa pamoja na Mbunge pia Mwenyekiti wa chama cha CCM (picha na Ezra Mwilwa)