Baraka FM

Machifu Mbeya wachafukwa TARI kulima juu ya makaburi

11 April 2024, 18:00

Chief mkuu wa kabila la Wasafwa Mbeya Roketi Mwashinga (kushoto)-picha na Josea Sinkala

Baadhi ya wananchi wa kata Ituha jijini Mbeya wamekerwa na kitendo cha Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI) kituo cha Uyole kuvamia maeneo yao waliozika ndugui zao.

Na Josea Sinkala

Serikali wilayani Mbeya imeanza mchakato wa kumaliza mgogoro wa ardhi unaoendeleo kati ya viongozi wa kimila (Machifu) na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI) kituo cha Uyole katika eneo la chuo cha kilimo jijini Mbeya.

Hatua hizo za kutatua mgogoro zimeanza kuchukuliwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mhe. Beno Malisa kwa kukutana na pande zote mbili, zenye mvutano juu ya eneo hilo ikiwa ni upande wa Machifu na upande wa TARI na kusikiliza hoja za pande hizo, ambapo machifu wanadai eneo la hekari nane walilotengewa sio eneo sahihi huku wakidai eneo lenye makaburi ya viongozi wao wa kimila waliofariki miaka kadhaa iliyopita ndio eneo sahihi wanalopaswa kukabidhiwa, lakini taasisi hiyo inatumia katika shughuli za Kilimo.

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mhe. Beno Malisa(picha na Josea Sinkala)
Sauti za baadhi machief Mbeya

Kwa upande wa kituo cha utafiti wa kilimo TARI wanadai kuwa eneo walilowapatia machifu ni eneo sahihi ambalo linawatosha kufanya shughuli zao za kimila ambapo gharama zimetumika kuweka uzio kwa ajili ya kulitambua eneo hilo na kwamba halitotumika kwa ajili ya shughuli za kilimo.

DC Malisa amezitaka pande zote mbili kuwa watulivu kwa kipndi hiki ambacho inatafutwa suluhu ya mgogoro huo na kusimamisha shughuli za kimila na kilimo katika eneo hilo mpaka pale ambapo utatuzi wa mgogoro utapatikana siku za hivi karibuni baada kamati ya uchunguzi kufanya kazi yake.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mhe. Beno Malisa