Baraka FM

Mbeya kupunguza maambukizi ya malaria ifikapo 2025

19 October 2023, 19:15

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Comrade Juma Homera akikabidhi chandarua kwa mmoja ya maafisa elimu mkoani mbeya(picha na mwandishi wetu)

Dunia imeendelea kupambana na ugonjwa wa maralia hivyo Tanzania kama nchi haina budii kuuangana na dunia katika kutimiza hilo,hali hiyo imefika mpaka ngazi za chini katika kuendeleza jitihada za kutokomeza maralia katika ngazi ya familia.

Na mwandishi wetu Mbeya

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Comrade Juma Homera amezindua rasmi Zoezi la Ugawaji Vyandarua vyenye Dawa kwa Wanafunzi Mashuleni ikiwa ni sehemu ya Mikakati na Mipango Madhubuti ya kuzuia, kuteketeza na kutokomeza kabisa Maralia kwa Mkoa wa Mbeya.

Vyandarua hivyo vimepokelewa na Maafisa Elimu Kutoka Halmashauri zote kwa niaba ya Wanafunzi na Kisha Zoezi la Uzinduzi na Ugawaji litaendelea katika Kila Wilaya na Halmashauri kwa Usimamizi wa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi kwa kishirikiana na Maafisa Elimu.

baadhi ya wakuu wa wilaya mkoa wa mbeya wakifuatilia kwa umakini zoezi la uzinduzi wa ugawaji wa vyandarua (picha na mwandishi wetu)

Zoezi hilo limefanyika katika Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa ambapo RC Homera ameshiriki katika kikao maalumu Cha kujadili, kupokea maoni na kushauri Njia mbadala za kuzuia na kutokomeza Ugonjwa huo hatari unaozidi kuua Maelfu ya Watu Duniani.

Katika Hotuba yake RC Homera amewaasa Maafisa Elimu kutoonyesha Upendeleo wa aina yeyote wakati wa Ugawaji wa Vyandarua hivyo bali Kila Mmoja apate kulingana na taratibu zilivyowekwa na Mamlaka husika.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Comrade Juma Homera akizunhgumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya mapambano ya maralia(picha na mwandishi wetu)

RC Homera amesema Zoezi hili la Ugawaji wa Vyandarua Mashuleni ni Adhima ya Serikali ya awamu ya sita kuhakikisha inapunguza maambukizi ya Maralia Kutoka Asilimia 8.1 Mwaka 2022 mpaka kufikia kiwango Cha Chini Cha Asilimia 3.5 ifikapo Mwaka 2025.Kikao hicho kilichofanyika Leo Oktoba 18 2023 kineshirikisha Wadau mbalimbali wakiwemo Wizara ya Afya, Wizara ya Elimu Wizara ya TAMISEMI, MSD Taasisi na Viongozi Kutoka Halmashauri zote za Mkoa wa Mbeya.