Baraka FM

Waislamu Mbeya wapewa tabasamu na MNEC Mwaselela

9 April 2024, 14:47

Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) kutoka Mkoa wa Mbeya Ndugu Ndele Mwaselela(aliyevaa shati ya kijani).

Jamii ina hitaji upendo,kila mtu anapaswa kumonyesha upendo mwingine hiyo kwa Mungu ni thawabu kubwa.

Na Mwandishi wetu

Kuelekea sikukuu ya Eid El-fitri Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) kutoka Mkoa wa Mbeya Ndugu Ndele Mwaselela ametoa sadaka ya Ng’ombe Mmoja na Kilo 100 za Mchele kwa waumini wa dini ya Kiislamu katika Msikiti Mkuu Jijini Mbeya.

Akikabidhi Sadaka hiyo kwa Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Sheikh Msafiri Njalambaha amesema chama cha Mapinduzi chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kinaamini kuwa kazi kubwa ya CCM ni kuwa karibu na jamii.

“Kazi yetu kama CCM na tunasisitizwa mara kwa mara na Mwenyekiti wetu wa Taifa Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa yatupasa kuwa karibu na jamii wakati wote” amesema M-NEC Mwaselela.

Kwa upande wake Sheikh Msafiri Njalambaha amemshukuru kiongozi huyo na kwamba sadaka hiyo itawagusa wahitaji ambao kuna Wakati nyakati za Sikukuu huwa wanakuwa hawajajaliwa kupata chochote.

Aidha amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwa na wasaidizi wake ndani ya CCM wanaojali watu.