Baraka FM

Zahanati ya Rufumbi wilayani Rungwe mbioni kukamilika

9 January 2024, 18:30

Na mwandishi wetu

Hatua ya ukamilishaji katika zahanati ya Lufumbi kata ya Masoko inatoa fursa kwa wakazi wa kijiji hiki kupata huduma ya matibabu karibu na makazi yao.

Zahanati hii imejengwa kwa nguvu za wananchi huku Halmashauri ikitoa kiasi cha shilingi Millioni 20 kwa kutumia Mapato yake ya ndani kwa ajili ya ukamilishaji.

Kijiji cha Lufumbi kipo takribani km 10 kutoka Tukuyu Mjini barabara ya Tukuyu- Mbila-Busisya na wakazi wake hupata matibabu katika zahanati ya Ngaseke, Masoko na Kalebela pamoja na Hospitali ya wilaya Tukuyu ” Makandana”