Baraka FM

Dkt.Nchimbi atua Mbeya kwa kishindo

16 April 2024, 16:58

Katibu Mkuu wa CCM Taifa Dkt. Emmanuel Nchimbi (aliyevaa skafu) akipokelewa na wenyeji wake baada ya kuingia katika ardhi ya mkoa wa Mbeya.

Katibu Mkuu wa CCM Taifa Dkt. Emmanuel Nchimbi ameendelea na ziara yake ya mkoa kwa mkoa na sasa ametua mkoani Mbeya baada ya kutoka kwenye ziara katika mikoa ya Katavi,Rukwa na Songwe.

Na Hobokela Lwinga

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Cde:Juma Z. Homera ameshiriki Zoezi la Mapokezi ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Balozi Dkt: Emmanuel Nchimbi ambaye amewasili Leo Mkoani humo kwaajiri ya Ziara ya Siku Mbili Wenye lengo la Kusikiliza na Kutatua Kero za Wananchi.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Cde:Juma Z. Homera(kulia)akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM Taifa Dkt.Emmanuel Nchimbi.

Katika Ziara yake Dkt: Nchimbi atazungumza na Wananchi Katika Halmashauri Tatu Tarhe 16 atazungumza na Wananchi wa Mji Mdogo wa Mbalizi Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, Tarhe 17 atakuwa na Mkutano wa Hadhara Uwanja wa Luanda Nzovwe Jiji la Mbeya na Tarhe 18 atazungumza na Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali.

Dkt: Nchimbi ameambatana na Katibu Wa Siasa Itikadi Uenezi na Mafunzo Taifa CPA Amos Makalla na Sekretarieti yake nzima.