Baraka FM

Askofu Panja: Tendeni mema ili mkumbukwe

21 November 2023, 19:34

Baadhi ya waombolezaji katika ibada ya kumuuga marehemu mch.sifaewl mwashibanda ushirikani Karasha Moravian(Picha na Hobokela Lwinga)

Na Hobokela Lwinga

Askofu mteule wa kanisa la Moravian Tanzania jimbo la kusini magharibi mch.Robart Pangani amewataka wananchi nchini kutunza amani iliyopo kuanzia kwenye maeneo yao wanayoishi  badala ya kuwa wavunjifu wa amani.

Hayo ameyasema katika ibada ya msiba wa kumuuga marehemu  mch.sifael mwashibada katika ushirika wa meta jijini mbeya .

Mch.Pangani amesema kila mwananchi anapaswa kuepuka makundi maovu yenye viashiria vya uvunjifu wa amani badala yake wanapaswa kuwa wanyenyekevu na kuomba toba kwa Mungu.

Askofu mteule wa kanisa la Moravian Tanzania jimbo la kusini magharibi mch.Robart Pangani(Picha na Hobokela Lwinga)
Sauti ya askofu mteule wa kanisa la Moravian Tanzania jimbo la kusini magharibi mch.Robart Pangani

Akihubiri katika ibada ya mazishi katika ushirika wa Karasha Mbozi Songwe askofu Keneni Panja wa kanisa la Moravian jimbo la kusini amesema kila mtu anapaswa kutenda ili aweze kukumbukwa duniani na mbinguni.

Askofu Keneni Panja wa kanisa la Moravian jimbo la kusini (Picha na Hobokela Lwinga)
Sauti ya askofu Keneni Panja wa kanisa la Moravian jimbo la kusini

Hata hivyo askofu wa makanisa ya Brotherhood Tanzania  askofu Rabi Mwakanani aliyefika katika ibada ushrikani  Meta kuungana na waombolezaji kumuuga mch.Mwashibanda amesema mch.Mwashibanda atakumbukwa kwa mambo mengi ikiwemo unyenyekevu na uchaji kwa Mungu.

Askofu wa makanisa ya Brotherhood Tanzania  askofu Rabi Mwakanani (Picha na Hobokela Lwinga)
sauti ya askofu wa makanisa ya Brotherhood Tanzania  askofu Rabi Mwakanani

Sambamba na hayo akisoma wasifu wa marehemu ,katibu wa kanisa la Moravian jimbo la kusini Magharibi ndugu Israel Mwakilasa amesema enzi za uhai wa mch.Mwashibanda amehudumu katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na shirikani,idara pamoja na taasisi za kanisa.

Katibu wa kanisa la Moravian jimbo la kusini Magharibi ndugu Israel Mwakilasa (Picha na Hobokela Lwinga)
Sauti ya katibu wa kanisa la Moravian jimbo la kusini Magharibi ndugu Israel Mwakilasa

Aidha viongozi wa mtaa wa Kajigili unapopatikana ushirika wa Meta wamesema kwao wamepata pengo kubwa kwani mchungaji huyo alikuwa mshauri mzuri katika kuchochea maendeleo kwenye mtaa huo.

Sauti za viongozi wa mtaa wa Kajigili

Mch.Sifael Mwashibanda amezikwa katika eneo la karasha Mlowo Mbozi mkoani Songwe na ameacha mjane na watoto sita.

Mjane wa marehemu mch Sifael Mwashibanda(katikati) bi, Anna mwakitalu(Picha na Hobokela Lwinga)